RC KUNENGE AZINDUA GARI YA AINA YA HONGYANG ILIYOUNGANISHWA HAPA NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge,(katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua gari aina ya Hongyang iliyounganishwa hapa nchini na mafundi wazalendo hapo Kibaha. 

RC Kunenge ameipongeza Kampuni ya GFA iliyofanya kazi hiyo na kuwataka maafisa wa serikali mkoani humo. "Mlianza kuunganisha magari ya FAO na leo mmeunganisha gari ya kwanza aina ya Hongyang ambayo iko katika muundo wa tipa, hongereni sana." Alisema.

RC Kunenge pia alitoa Rai kwa taasisi za Serikali mkoani humo kutokuwa kero kwa wawekezaji na biashara zao badala yake ziwasaidie ili kutekeleza vema SHERIA za nchi.

"Sintopenda na sintaruhusu kila siku Afisa wa serikali anatembelea kiwanda au biashara asubuhi mpaka jioni, waacheni wafanye kazi na sisi serikali tuwasaidie kuweka mazingira mazuri ili waweze kutekeleza SHERIA zilizopo na sio kuwa keep." Alionya RC Kunenge.




 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"