Saturday, June 19, 2021

RC KUNENGE AENDELEA KUWAPIGANIA WAWEKEZAJI MKOA WA PWANI

 Mhe. Abubakar Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Pwani leo  Juni19, 2021  amekutana na Wawekezaji na Wafanyabiashara Mkoa wa Pwani katika Kikao cha Baraza la Biashara Mkoa, 

Mhe. Kunenge Amezipa Mwezi Mmoja  Taasisi za Serikali zinazohusika na Kuhudumia Wawekezaji   Mkoani  Pwani kuhakisha mipango yao ya kupeleka  huduma Viwandani inafahamika na Wawekezaji na inakidhi mahitaji yao.  "Lazima Taasisi za Serikali Mkoani Pwani Mipango yao iendane na Ramani  ya Uwekezaji ya Mkoa"

Kunenge, Ameeleza kuwa amedhamiria kubadilisha Pwani amewataka  Watendaji Mkoani humo kuhakisha kuwa Vikwazo vyote kwa Wawekezaji  vinashughulikiwa kwa Wakati, Ameagiza kuimarishwa kwa Dawati la Uwekezaji Mkoa ambalo litakuwa likifuatilia maendeleo ya Wawekezaji kila siku.

Kunenge Ametoa rai kwa vishoka wanaovamia na kuuza ardhi na wote  wanaochochea migogoro ya Ardhi Mkoani hapo kuacha Mara moja,  Ameunda  timu ya kutatua Migogoro ya Ardhi Mkoani Pwani ambayo pia ni kikwazo cha Uwekezaji. Kunenge Amezitaka Taasisi za Serikali Mkoani hapo  kuacha kusumbua wawekezaji kwa kaguzi za mara kwa mara ambazo hazina Tija, "Wawekezaji siku nzima wanapokea Watendaji wa Serikali kwa kaguzi watatanya kazi saa ngapi?"alisema Kunenge.

Kunenge Ameahidi, kufanyia Kazi Changamoto zote za Uwekezaji na kuwapa Mrejesho, ahaidi Ushirikiano  kwa Wawekezaji ili kukuza Uwekezaji wao. Azitaka Taasisi za Umma kuimarisha Mahusiano mazuri na Wawekezaji ili kuongeza  ukusanyaji Kodi, kukuza Biashara zao, kuongeza  Ajira.

Kunenge ameagiza kufanyika kwa Mabaraza ya Biashara ya ngazi ya Wilaya, ameziagiza pia Halmashauri kupanga miji ili kuvutia uwekezaji.
0 comments:

Post a Comment