MKURUGENZI WA MASHTAKA (DPP) AWAFUTIA MASHTAKA YA UGAIDI YALIYOKUWA YAKIWAKABILI MASHEIKH, WENGINE TAYARI WAMEUNGANA NA FAMILIA ZAO


Sheikh Farid Ahmed (wa pili kushoto) akiwa nyumbani kwake mjini Unguja, Zanzibar mara baada ya kuachiwa huru. Farid ni miongoni mwa masheikh 36 wa uamsho ambao walikuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za ugaidi kwa zaidi ya miaka 9 ambapo leo DPP ameyafuta mashtaka hayo na kuwaachia huru.
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Sylvester Mwakitalu amesema kuwa amewafutia mashitaka masheikh wote 36 wa Uamsho na kwamba tayari wengine waliachiwa toka jana na wengine wanasubiri taratibu za kutoka gerezani.
Sheikh Ponda Issa Ponda kulia, anae fatia ni Sheikh Mselem Ally bingwa wa tafsiri ya Qur'an Afrika Mashariki wakiwa nyumbani kwa Sheikh Mselem muda huu baada ya kuachiwa hapo jana.
 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"