MSONGAMANO WA MALORI BANDARINI: WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA MAAGIZO

*Aagiza dosari za mfumo wa TANCIS zishughulikiwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mamlaka ya Bandari Tanzania na Mamlaka ya Serikali Mtandao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Mei 12, 2021) alipotembelea bandari ya Dar es Salaam ili kuona utendaji wa bandari hiyo.

“TPA endeleeni kuiimarisha bandari yetu, hii ni sura ya uchumi wa nchi yetu, zungumzeni lugha moja ya uwajibikaji, TRA muwepo maeneo yote yanayohitaji uwepo wenu na muda wote wateja wetu wahudumiwe ili bandari yetu iendelee kuwa bora. Nchi nyingi zinatutegemea”

Amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ihakikishe mfumo wa pamoja wa forodha Tanzania (TANCIS) unafanya kazi kwa ufanisi ili kupuinguza malalamiko ya wateja kuhusu mfumo huo.

“Dosari zote za mfumo wa TANCIS zifanyiwe kazi, mfumo usituharibie, mnapoona kuna madhaifu fanyeni marekebisho ya haraka, tunataka wateja waingie na kutoka kwa muda mfupi” Amesema.







 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"