5/11/2021

DKT. MWIGULU NCHEMBA AIAGIZA TIRA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA BIMA NCHINI

 Na Farida Ramadhani - WFP , Dodoma


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili kuongeza wingo wa huduma za bima nchini.

Ametoa agizo hilo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), walipokwenda kujitambulisha na kutoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo ofisini kwake jijini Dodoma.

“Tunataka taasisi za Serikali zinazosimamia sekta mbalimbali za biashara na uwekezaji ikiwemo nyinyi TIRA kuwa wawezeshaji wa biashara hizo kuendelea kufanyika bila kikwazo”, alibainisha Mhe. Dkt. Nchemba.

Kwa upande wake, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Dkt. Mussa Juma alimuahidi Mhe. Waziri kuwa taasisi hiyo itayafanyia kazi maagizo hayo kwa kuhakikisha changamoto zote zinapatiwa ufumbuzi ili kuimarisha sekta hiyo na kukuza uwekezaji.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimsikiliza Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja wakati wa kikao na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akitoa maagizo kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) wakati alipokuwa na kikao na baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo ambayo iko chini ya Wizara hiyo, jijini Dodoma.

Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Zanzibar, Bi. Khadija Issa Said akimuelezea wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) idadi ya Kampuni za Bima zilizosajiliwa na TIRA nchini, jijini Dodoma.



Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), jijini Dodoma.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) walipofika ofisini kwake jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimsikiliza kwa makini Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Mussa Juma wakati alipofanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo, jijini Dodoma.


Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Mussa Juma akimuelezea Akimuelezea wa kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) majuku ya TIRA wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma)
    

0 comments:

Post a Comment