WAKAZI 70 WA KATA YA UHAMAKA WAPATA MAFUNZO YA KUPAMBANA NA UKATILI.

 

Afisa Mradi  wa Shirika  lisilo la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL)Mkoa wa Singida, Philbert Swai, akielekeza jambo katika  mafunzo ya kuwawezesha vijana kupambana na ukatili wa kijinsia yaliyofanyika juzi Kata ya Uhamaka.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Edna Mtui akitoa mada.
Mratibu wa mradi wa kutokomeza ukatili na ukeketaji kutoka Shirika hilo,   Annamaria Mashaka akitoa mada katika mafunzo hayo.
Vijana wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Elizabeth Haji akitoa mada.
Mafunzo yakiendelea.
Mkunga wa Jadi, Monica Irumba, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Rajab Chagama akitoa mada.
Mwakilishi wa kundi la vijana, Zainabu Kijanga, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, John Nzungu akitoa mada.
Washiriki wa Kundi la Vijana wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo.
Viongozi wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida.


VIONGOZI wa dini wamewataka wazazi kutowaruhusu na kuwaelekeza watoto wao mambo ya kufanya na yale yasio wapasa kuyafanya kuliko kuogopa wakidhani kufanya hivyo ni kuwajengea tabia mbaya.

Hayo yalisemwa jana na viongozi hao katika Kata ya Uhamaka Manispaa ya Singida walipokuwa wakipatiwa mafunzo ya kuwawezesha kupambana na ukatili wa kijinsia yanayotolewa na Shirika lisilokuwa la Serikali la Empower Society Transform Lives (ESTL) la mkoani hapa.

Katika Mafunzo hayo yaliyoshirikisha makundi mbalimbali yenye zaidi ya watu 70 ya vijana, wakunga wa jadi, mangariba wastaafu,watu maarufu pamoja na viongozi wa dini ndani ya kata hiyo, Viongozi hao walieleza bayana kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa kuwa wakiwaachia uhuru sana watoto wao na kupelekea kujifunza mambo yasiyofaa ambayo yanakuja kuzaa vitendo vya ukatili.

"Wapo wazazi hasa wa kike wanatumia hizi simu kubwa angali hawajui vitu vingi vilivyopo kwenye hiyo simu,kuitumia hiyo simu sio shida lakini unakuta mtoto ndio anajua vitu vingi kwenye Simu ya Mzazi mpaka Video za Ngono na mzazi yupo anaangalia baada ya siku utasikia amebaka ama amepata ujauzito kabla ya wakati."

Aidha waliomba viongozi kwenye nyumba zao za ibada kukemea kwa nguvu zote na kutoruhusu ndoa za utotoni huku wakiwafundisha waumini wao bila kuogopa mambo yasiyofaa kwenye jamii bila kuyaficha ficha ili kuokoa na kujenga jamii itakayo kuwa na maadili mema.

 Monica Irumba ambaye ni Mkunga wa Jadi alisema kukosekana kwa elimu kwa wazazi ni chanzo mojawapo ya kuendelea kuwepo ukatili wa kijinsia kwani wazazi wengi wanaishi kwa mazoea ndio maana wengine ukiwauliza kwanini anamkeketa mtoto atakwambia nimekuta bibi yangu anafanya hivi.

"Niwaombe wazazi wenzangu tuishi kwa upendo, upendo ukikosekana ndio inapelekea kuwepo Vitendo vya ukatili,tuache mazoea,tuachane na mila zisizofaa." alieleza Monica kwa uchungu.

ESTL imeendelea kutoa mafunzo mbalimbali ya kuiwezesha jamii kupambana na ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yao kupitia mradi wao wa kutokomeza ukatili na ukeketaji mradi unaofadhiliwa na Ubalozi wa Finland hapa nchini ukitekelezwa na Shirika hilo chini ya Mratibu Annamaria Mashaka.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"