4/16/2021

TANESCO KANDA YA KATI YATOA MAFUNZO KWA WAHANDISI WA MIKOA YA SINGIDA, DODOMA NA MOROGORO

 

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Reymond Seya, akitoa maelekezo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Wahandisi (Engineer Forum) kutoka  Mikoa ya Singida Dodoma na Morogoro mkoani hapa leo.
Wahandisi wote wa Tanesco  Kanda ya Kati wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),  Mhandisi,  Reymond Seya.
Meneja Mwandamizi wa Usambazaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),  Athanasius Nangali, akitoa mafunzo kwa wahandisi hao.
 


Na Mwandishi Wetu, Singida


SHIRIKA la Umeme Kanda ya Kati (Tanesco) limetoa mafunzo ya siku tatu kwa Wahandisi (Engineer Forum) kutoka Mikoa ya Singida Dodoma na Morogoro.

Mafunzo hayo yanayofanyika mkoani hapa, yamelenga kuongeza ufanisi kwenye ufanyaji kazi za kila siku.

Akifungua mafuzo hayo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji na Huduma kwa Wateja  wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Reymond Seya,  alisema wahandisi ni watu muhimu sana katika ustawi wa uchumi wa Taifa.

"Sisi kama shirika la umeme hapa nchini lazima tuhakikishe umeme haukatiki katiki hovyo ili uchumi wa nchi yetu usonga mbele, nendeni mkafanye kazi kwa bidii." alisema Seya.

Akiendesha mafunzo hayo Meneja Mwandamizi wa Usambazaji wa shirika hilo,  Athanasius Nangali alisema wapo hapo kwa ajili ya kupitia na kutazama majukumu yao kwenye utendaji wa kazi na kwamba baada ya mafunzo hayo watakwenda kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wateja wanapata umeme wa uhakika.

    

0 comments:

Post a Comment