RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AREJEA DAR ES SALAAM

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaam leo APRILI 8, 2021 AKITOKEA Zanzibar alikokwenda kwenye dua ya kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Sheikh Abeid Aman Karume. Kwenye Uwanja wa ndege wa Aman Karume Zanzibar, Rais alisindikizwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah na KATIBU Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Said, wakati kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Rais Samia alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Aboubakar Kunenge.




Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"