RAIS SAMIA ASHIRIKI KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI LA KUOMBEA TAIFA NA KUMSHUKURU MUNGU KWA MAISHA YA HAYATI DKT JOHN POMBE MAGUFULI JIJINI DODOMA LEO

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali akishiriki kuomba dua kabla ya kuanza kwa Kongamano la Viongozi wa Dini la Kuomuombea na Kuombea Taifa pamoja na kumshukuru Mungu kwa ajili ya Maisha ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma leo Jumapili Aprili 18, 2021.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Aprili 18, 2021 ameungana na Viongozi mbalimbali wa Dini na Watanzania katika Kongamano la Viongozi wa Dini la kumshukuru Mungu kwa maisha ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma.






Baadhi ya watu wakifanya maombi ya Dua na Sala maalum katika Kongamano la Viongozi wa Dini la kumshukuru Mungu kwa maisha ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma na Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.











Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"