WANAWAKE TANESCO WATOA MSAADA, WAWAFUNDA WASICHANA SHULE YA KONDOA.

 

Katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani, Wafanyakazi wanawake wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Makao Makuu, wametoa msaada na kuwafunda wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa. 

Afisa Mkuu wa fedha TANESCO, CPA. Renata Ndege amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa kuwa chachu ya maendeleo kwa kuzingatia elimu, nidhamu na upendo ili kufikia malengo yao. 

Wanawake kutoka TANESCO Makao Makuu wametembelea shule hiyo ya wasichana Kondoa iliyopo Mkoani Dodoma Tarehe 07.03.2021 

Katika hafla hiyo Mwenyekiti wa TANESCO wanawake Makao Makuu, Bi. Prisca Maziwa alisema umoja wa wanawake wameamua kuja kusherekea siku hiyo katika shule ya wasichana Kondoa. 

"tumewaletea vifaa mbalimbali kama Magodoro, Mashuka, Mito, Chandarua, dawa na vifaa vya usafi kwaajili ya Zahanati ya shule" Bi. Maziwa

Pia aliongezea kua shirika liliweza kutoa vitabu vya masomo mbalimbali, jezi za michezo, taulo za kike kama ishara ya kusherekea siku hiyo muhimu ya kina mama duniani.

Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Kondoa Bi. Flora Msuya amewashukuru wanawake wa TANESCO kwa upendo  wao kwa kuweza kuwachagua kushiriki nao katika siku ya wanawake na kuwaletea msada wa takribani milioni sita.

Aidha, wanafunzi wa Shule ya sekondari ya wasichana Kondoa nao walishukuru wanawake wa TANESCO kwa upendo wao na kuahindi kuutumia msada waliopata vizuri na kuongeza juhudi katika masomo yao.

Shule ya sekondari wasichana Kondoa ina takribani ya wanafunzi 680 katika michepuo ya sanaa na sayansi, ambapo kwa miaka mitatu mfululizo imekua ina ufaulu wa asilimia tisini na tisa.

hii ilikua jana

















Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"