Friday, March 5, 2021

RC KUNENGE ATAKA KIPAOMBELE CHA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA KUZINGATIA MAHITAJI YA WANANCHI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka wajumbe wa Bodi ya Barabara kuhakikisha vipaombele vya Ujenzi wa Barabara vinazingatia mahitaji ya wananchi.

RC Kunenge amesema hayo wakati wa kikao Cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam ambapo amesema kumekuwa na ujenzi wa Barabara ambazo sio kipaombele Cha wananchi na kuacha zile zenye uhitaji zikibaki kuwa mbovu Jambo linalosababisha kero kwa watumiaji.

Kutokana na hilo RC Kunenge amesema kuanzia sasa ikitokea vikao vimepitisha Mambo yasiyozingatia mahitaji ya wananchi walio wengi yakifika mezani kwake hatoyaidhinisha kwakuwa ameamua kuwa sauti ya walio wengi.

Katika hatua nyingine RC Kunenge ameonyesha kuchukizwa na tabia ya baadhi ya Viongozi wanaochelewa kuhudhuria kwenye vikao na kusababisha vikao kuchelewa kuanza kitendo alichokiita utovu wa nidhamu.0 comments:

Post a Comment