KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, WANAWAKE WA TUGHE WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAPANDA MITI MJI WA SERIKALI, MTUMBA JIJINI DODOMA

Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Wizara ya Fedha na Mipango wakipeleka miti katika eneo la upandaji katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mtumba jijini Dodoma kuelekea sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Gisela Mugumira akipanda mti katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yanayotarajiwa kufanyika Machi 8, 2021.

Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Agatha Madalle akisawazisha udongo baada ya kupanda mti katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yenye kaulimbiu ya “Wanawake katika uongozi chachu kufikia Dunia yenye usawa”.

 

Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Gisela Mugumira (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Agatha Madalle (kulia) wakijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe wa TUGHE wakati wa zoezi la upandaji miti katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya kutunza mazingira ikiwa ni maandalizi ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.

 

Afisa Tawala wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Haika Mlay na Mjumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) wa wizara hiyo, Bi. Husna Hamis wakishirikiana kupanda mti katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"