Wednesday, March 31, 2021

DKT. PHILIP MPANGO AAPISHWA KUWA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA

DKT. Philip Isdor Mpando ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Alasiri Machi 31, 2021.

Mhe, Mpango ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

Pia katika hafla hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  MheHemed Suleiman na Spika wa Bunge Mher. Job Ndugai sambamba na viongozi wa juu wa serikali.

Dkt. Mpango alikuwa WAZIRI wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hajamteua kushika wadhifa huo.

 

0 comments:

Post a Comment