2/25/2021

TANESCO YAKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME KWA AJILI YA SGR KWA ASILIMIA 99

NA K-VIS BLOG, KINGURUWILA
MRADI wa ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa ajili ya treni ya umeme maarufu kama SGR umekamilika kwa asilimia 99, Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Nchini TANESCO Mhandisi Albano Mahimbo amesema leo Februari 25, 2021 mjini Morogoro.
Alisema kazi ambazo zimekamilika ni kupanua kituo cha kuzalisha umeme Kinyerezi jijini Dar es Salaam kwa kujenga Switch-yard sehemu ya kuchukua umeme na kujenga njia ya kusafirisha umeme (transmission line) kutoka Kinyerezi hadi Kinguruwila mkoani Morogoro.
“Kuanzia Kinyerezi hadi Kinguruwila tumejenga nguzo 462 zinazohitajika lakini pia tumeshavuta waya katika nguzo zote 462.”
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kwenye eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kwa ajili ya matumizi ya SGR eneo la Kinguruwila mjini Morogoro, Mhandisi  Mahimbo alisema kazi hiyo ilianza Januari 24, 2019 na hadi Desemba 12, 2020 kazi zote zilikuwa zimekamilika.
Akifafanua kuhusu mahitaji ya umeme kwa ajili ya SGR  alisema mahitaji halisi ni Mehawati 70 lakini mradi huo una uwezo wa kubeba Megawati 500.
Akizungumzia upatikanaji wa uhakika wa umeme kwa ajili ya SGR Mhandisi Mahimbo alisema, TANESCO katika mradi huo imejipanga vizuri na kwamba kutakuwa na vituo vinne (traction Power Stations) vya kupoza umeme kutoka Kilovolti 220 hadi Kilovolti 27.5 ambayo ndiyo mahitaji ya kuendesha treni ya umeme.
“Tutakuwa tuna umeme unaotoka Kinyerezi kuja hapa Kinguruwila, kutakuwa na umeme unaotoka Morogoro kuja hapa Kinguruwila, kutakuwa na umeme unaotoka Ubungo hadi Kinguruwila hivyo kama kuna sehemu moja ya kusafirisha umeme ina shida sehemu nyingine itafanya kazi ya kufikisha umeme hapa Kinguruwila hatutarajii itakuja kutokea reli yetu ya SGR haina umeme.” Alisisitiza.

Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Nchini TANESCO Mhandisi Albano Mahimbo, akizungumza na wahariri eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kwa ajili ya SGR (traction power station) eneo la Kinguruwila mkoani Morogoro leo Februari 25, 2021.
Kituo cha kupoza umeme kwa ajili ya SGR (traction power station) eneo la Kinguruwila mkoani Morogoro Kama kinavyoo ekana leo Februari 25, 2021.
Kituo cha kupoza umeme kwa ajili ya SGR (traction power station) eneo la Kinguruwila mkoani Morogoro kikiwa pem ezoni mwa reli ya treni ya umeme Kama kinavyo onekana leo Februari 25, 2021

Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Nchini TANESCO Mhandisi Albano Mahimbo, (kushoto) akizungumza na wahariri eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kwa ajili ya SGR (traction power station) eneo la Kinguruwila mkoani Morogoro leo Februari 25, 2021.
Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Nchini TANESCO Mhandisi Albano Mahimbo.

    

0 comments:

Post a Comment