NA
K-VIS BLOG, MOROGORO
WAZIRI
wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani amesema Serikali kupitia TANESCO tayari
imetenga Megawati 70 za umeme wa kuendesha treni ya mwendokasi maarufu SGR.
Mhe.
Dkt. Kalemani ameyasema hayo leo Februari 27, 2021 wakati akifungua rasmi kikao
kazi cha TANESCO na Wahariri wa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa NSSF mkoani
Morogoro.
Mahitaji halisi ya kuendesha treni hiyo ya umeme ni Megawati 27.
“Tunampongeza
sana Rais wetu kwa kuamua kujenga SGR, hata treni hiyo ingekuwa tayari leo
treni hiyo ingeendeshwa kwa umeme bila mashaka yoyote.” A.lisisitiza.
Alisema
tayari miundombinu ya umeme kiasi cha kilomita 160 ikiwa ni pamoja na kuweka
nguzo na nyaya za umeme kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro imekamilika na
kwamba kinachosubiriwa ni kuiunganisha treni hiyo na umeme wa TANESCO.
Akizungumzia
hali ya umeme nchini kwa sasa, Mhe. Waziri amewahakikishia watanzania na
wawekezaji wa ndani na nje kuwa umeme wa kuhakikisha unaendesha uwekezaji wao
upo wa kutosha na wa uhakika.
“Kwa
sasa tuna jumla ya Megawati 1,604.28 za umeme huku mahitaji yetu ya umeme
nchini kwa siku ni Megawati 1,180 na kwa maana nyingine tuna ziada ya umeme
Megawati takriban 300.” Alifafanua Dkt. Kalemani.
Akizungumzia
Mradi mkubwa wa Kimkakakti wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP2115), Mhe.
Waziri alisema, ujenzi eneo la mradi unaendelea usiku na mchana chini ya
usimamizi wa TANROADS na TANESCO.
Alisema
mradi huo ambao unafadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali kwa thamani ya
Shilingi Trilioni 6.5 ni wa kwanza kwa ukubwa katika nchi za Afrika Mashariki
na wanne kwa ukumbwa barani Afrika, utaleta manufaa makubwa siyo tu ya
kuzalisha umeme bali pia utunzaji wa mazingira, kilimo cha mseto, umwagiliaji
na ufugaji.
“Kwa
sasa watanzania tunatumia mkaa na kuni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mathalan
Dar es Salaam pekee kwa mwaka inatumia magunia msi chini ya magunia 400,000
hadi 500,000 kwa mwaka ambayo ni sawa na heka 1 ya miti.” Alifafanua.
Kwa
hiyo umuhimu wa mradi huu utawawewezesha Watanzania kutumia nishati ya umeme
kwa m atumizi ya nyumbani kwasababu mradi utakapokamilika gharama za umeme
zitashuka sana, alibainisha Dkt. Kalemani.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtedaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka alisema madhumuni
ya kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari ni kuwapa fursa ya kujenga
uelewa wa shughuli mbalimbali za TANESCO hususan namna inavyotekeleza miradi
mbalimbali kwa niaba ya Serikali ukiwemo mradi mkubwa w akimkakati w aumeme wa
maji wa Julius Nyerere JNHPP2115.
“Lkani
Pia tuna miradi kama vile Rusumo (MW 87) ambapo hadi sasa utekezwaji wake
umefikia asilimia 76.8 na utagarimu kiasi cha shilingi billioni 263.
Hata
hivyo Serikali kupitia TANESCO, inatarajia kutekeleza miradi mingine mikubwa
kama vile Ruhuji 358 MW, Rumakali 222MW, Mtwara MW 300, Somanga fungu MW 300, Kakono
MW 87, Malagarasi 45 MW.” Alisema Dkt. Kalemani.
Dkt.
Mwinuka alisema Kupitia utekelezaji huu wa Miradi hii ya uzalishaji umeme,
tunategemea hadi kufikia 2025 TANESCO kuwa na uwezo wakuzalisha Megawati 5,000.
Hii itasidia Nchi kuwa na umeme wa kujitosheleza na utakaochochea ukuwaji wa
uchumi na kuuza ziada itakayobakia nje ya Nchi.
Kwa
upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abassi alisema “Nasimama hapa leo
kuwapongeza sana TANESCO kwani ni miongoni mwa taasisi za umma zinazotekeleza
wajibu wa kutoa habari kwa umma kikamilifu kwani ni haki ya kikatiba.
“Kila
taasisi zinapaswa kutoa habari kwa kukutana na waandsihi wa habari kuwapeleka
kwenye shughuli zao na miradi mbalimbali ili wananchi waweze kujua Serikali yao
inavyowahudumia na tunakwenda kuzipima na kuzitathmini taasisi zote za umma ili kuja zinavyotekelza wajibu huu wa kikatiba.” Alisema.
Hata hivyo Dkt. Abbasi amewaasa waandishi kuzingatia misingi na kanuni za uandishi wa habari ili wajikite kwenye jukumu la msingi la kutoa habari kwa manufaa ya umma na kujiepusha na uandishi wa habari za kizandiki na uzushi.
"Silaha kuu ya mwandishi wa habari katika kutekelza majukumu yake ni kuandika ukweli na sio uzushi." Alifafanua.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abassi akitoa mada kuhusu wajibu wa vyombo vya habari
0 comments:
Post a Comment