2/26/2021

MIKOA 16 TANZANIA BARA INA MAENEO YENYE VIASHIRIA VYA JOTOARDHI

NA K-VIS BLOG, MOROGORO

MIKOA 16 Tanzania Bara ina maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi vipatavyo 50, Meneja Mkuu, Kampuni Tanzu ya TANESCO ya Jotoardhi, Tanzania Geothermal Development Company Limited  (TGDC), Mhandisi Kato Kabaka (pichani juu)  amesema.

Mhandisi Kabaka ameyasema hayo leo Februari 26, 2021 Kikao Kazi cha TANESCO na Wahariri Waandamizi wa vyombo vya habari  kinachofanyika kwenye ukumbi wa NSSF mjini Morogoro 

Mhandisi Kato ameitaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Arusha, Dodoma, Iringa, Pwani, Kilimanjaro, Kagera, Katavi na Mbeya.

Mikoa mingine aliitaja kuwa ni pamoja na Shinyanga, Morogoro, Mara, Manyara, Rukwa, Singida, Songwe na Tanga.

“Maeneo hayo mengi yanapatikana katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki ambalo linapita hadi Kenya na inaelezwa kuwa katika bonde hilo kuna takriban 15,000MW za jotoardhi na wenzetu Kenya tayari wanazalisha zaidi ya 700MW za Jotoardhi na umeme 800MW.” Alisema na kuongeza kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na zaidi ya Megawati 5,000 za jotoardhi na kulingana na miradi iliyopo hivi sasa, tunatarajia kuzalisha umeme unaotokana na jotoardhi 200MW ifikapo 2025” Alibainisha Mhandisi Kato.

    

0 comments:

Post a Comment