ZIMAMOTO YAKABILI MATUKIO 9,035 YA MOTO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Khamis Hamza Chilo (Mb) akisisitiza jambo katika kikao alichokifanya na viongozi waandamizi na maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenye ziara ya kikazi katika ofisi za makao makuu ya Jeshi hilo Jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, 17 Januari, 2021.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limefanikiwa kuzima moto katika matukio 9,035 na kufanya maokozi 2,982. Akizungumza leo katika Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb) Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF John William Masunga alisema matukio hayo ni katika kipindi cha miaka mitano kuanzia (2015/16 – 2020/21).

Mh. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amefanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma na kupokea taarifa za vitengo mbalimbali kutoka kwa Kamishna Jenerali John Masunga.

Akizungumza mbele ya Viongozi waandamizi na Maafisa wa Zimamoto, Mheshimiwa Naibu Waziri alilipongeza Jeshi hilo kwa kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo namna wanavyokabiliana na matukio ya moto na maokozi mbalimbali. Mheshimiwa Naibu Waziri pia aliwasihi kuongeza juhudi katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika majanga ya moto pamoja na maokozi. “Kumekuwa na manung’uniko mbalimbali kutoka kwa wananchi kuwa mnachelewa kufika kwenye matukio pamoja na kwenda bila maji, sasa nawataka mkafanye kazi ili wananchi wafurahie huduma yenu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwapa elimu ya Kinga na Tahadhari dhidi ya Majanga ya Moto”

Mheshimiwa Naibu Waziri alianza Ziara yake kwa kukagua Mitambo ya Kuzima Moto Pamoja na vifaa muhimu vinavyotumika katika kuzima moto na kufanya maokozi mbalimbali katika ofisi za Kamanda (M) Dodoma zilizopo jirani na Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Mtaa wa Makole jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Khamis Hamza Chilo (Mb) Akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga, Makao Makuu Jijini Dodoma katika Ziara ya kikazi mapema leo asubuhi.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga akisoma taarifa ya Jeshi hilo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Khamis Hamza Chilo (Mb) alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dodoma mapema leo asubuhi.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao katika ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb) kilichofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jijini Dodoma hii leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb) akipata maelekezo ya matumizi ya vifaa mbalimbali vinavyotumika katika matukio ya moto na maokozi kwenye ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb) akipata maelekezo ya matumizi ya vifaa mbalimbali vinavyotumika katika matukio ya moto na maokozi kwenye ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dodoma.(Picha na Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji)
 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"