WAZIRI MKUU ATOA AGIZO UENDELEZAJI ZAO LA MKONGE

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Jumatano, Januari 20, 2021 amekagua kitalu cha miche ya mkonge cha TARI Mlingano kilichopo wilayani Muheza, Tanga na kufungua zoezi la ugawaji wa miche kwa wakulima wa zao hilo.

Akizungumza wakati wa tukio hilo Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge watenge ekari 10 kwa ajili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa miche ya mkonge.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itenge fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kituo cha TARI Mlingano ili kukiwezesha kupanua eneo la uzalishaji miche kwa kununua vitendea kazi yakiwemo matrekta.

Amesema kituo cha TARI Mlingano kinatakiwa kijikite katika kufanya  utafiti wa mbegu bora pamoja na dawa za kudhibiti magonjwa katika zao hilo na suala la uzalishaji wa mbegu lifanywe kwa ushirikiano katika ya kituo hicho na wadau wa zao hilo.






Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"