1/26/2021

TMDA YAITAKA JAMII KUACHA MARA MOJA UTEKETEZAJI HOLELA WA DAWA ZISIZO SALAMA


Mkaguzi wa Dawa kutoka TMDA Kanda ya Ziwa Mtani Magesa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali waliotembelea maabara hiyo iliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Kanda ya Ziwa Sophia Mziray akifafanua jambo kuhusu uteketezaji wa dawa zilizokwisha muda wake.

Baadhi ya mashine zinazotumiwa na wachunguzi wa maabara hiyo.

 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika maabara ya TMDA mkoani Mwanza wakati alipotembelea katika maabara hiyo kwa lengo la kupata taarifa ya  mambo mbalimbali yanayofanywa katika maabara hiyo.

Hili ndilo jengo la  Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) lililoko Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza eneo la Buzuruga.

........................................................... 

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kanda ya Ziwa imetoa wito kwa jamii kuepuka uteketezaji kiholela wa dawa zisizo salama na zilizokwisha muda wake katika mazingira ya makazi ili wafuate utaratibu elekezi toka kwa mamlaka hiyo.

Wito huo umetolewa na Mkaguzi wa Dawa kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa Bw.Mtani Magesa mbele ya waandishi wa habari waliotembelea ofisi hizo jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, amesema uteketezaji wa dawa lazima ufanyike kwa mujibu wa Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba na mwongozo wa uteketezaji wa dawa wa Mwaka 2009.

"Zipo dawa ambazo zikichomwa moshi wake huathiti watu na mazingira, hivyo uteketezaji dawa zilizotambulika kuwa siyo salama ama zimekwisha muda wake lazima zifuate utaratibu na kusimamiwa na TMDA," alisisitiza Magesa.

Magesa ameeleza: "Dawa nyingi tunazoteketeza kwenye eneo letu tunatumia kinu cha hospitali ya Bugando...zahanati na vituo vya afya wana dohari za kuteketezea dawa zisizo salama, zikiwemo zile ambazo zinabaki majumbani baada ya matumizi (leftovers)."

Mkaguzi huyo ametoa rai kuwa haipaswi kuteketezwa dawa kwenye eneo la wazi hata kama hawakai watu, mvua ikinyesha huweza kupeleka mabaki ya dawa ile kwenye maeneo ya watu au ziwani na kuathiri samaki ambao tunawatumia kama chakula."

Kwa upande wake Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Sophia Mziray TMDA imeendelea kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja wake, na kuongea udhibiti kwa kufuata mfumo na taratibu za ndani za utoaji huduma bora Ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ISO 9001:2015 na ISO/IEC 17025:2005.

"Kanda ya Ziwa inatekeleza majukumu yake kiudhibiti ikiwemo ukaguzi wa maeneo yanayozalisha, yanayouza, yanayohifadhi na kutoa huduma ya dawa, vifaa tiba, vitendanishi na vipukusi kwa mujibu wa Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba Sura namba 219," amefafanua Mziray.

Amewasihi wananchi kuendelea kushirikiana na TMDA ili kujua namna nzuri ya uendeshwaji wa shughuli zake, udhibiti wa dawa, vifaa Tiba na vitendanishi ikiwemo kutambua zaidinkuhusu uteketezaji wa dawa zisizo na ubora kwa lengo la kulinda afya ya jamii.

Mziray amesema mamlaka imekuwa ikifanya ukaguzi kabla ya kubaini nakuziteketeza dawa zisizo salama, ukaguzi huo unalenga kujihakikishia kuwa bidhaa zinaendelea kuzalishwa, kuhifadhiwa, kutunzwa vizuri na kutokea kwa utaratibu zikiwa na ubora, salama na zenye ufanisi.

Kanda ya ziwa inajumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga Kagera, Simiyu na Mara.

    

0 comments:

Post a Comment