Sunday, January 24, 2021

SIMBA YATANGAZA KOCHA MPYA, NI MFARANSA DIDIER GOMEZ


Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC, imemtangaza Mfaransa Didier Gomez kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kuanzia leo JANUARI 24, 2021.Akimtangaza kocha huyo mbele ya waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Jumapili Januari 24, 2021, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo ambayo umefanikiwa kuingia hatua ya makundi michuano ya Klabu Bingwa Barani Afria, amesema Gomez anachukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa Mabingwa hao Mbeleji Sven Vandenbroack aliyeamua kuachana na Simba hivi karibuni.

"Gomez ataongoza benchi la ufundi akisaidiwa na Selemani Matola.". Alisema Barbara Gonzalez CEO wa Simba.

Katika mazungumzo yake kocha huyo alisema anaifahamu Simba na anajua matamanio ya Klabu hiyo katika ushiriki wa michuano ya kombe la Mabingwa barani Afrika lakini pia ligi kuu ya Tanzania Bara.
 

0 comments:

Post a Comment