RC KUNENGE AFUNGUA WIKI YA SHERIA KANDA YA DAR ES SALAAM NA MIAKA 100 YA MAHAKAMA KUU NA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA YA MSAADA WA KISHERIA BURE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amefungua mahadhimisho ya Wiki ya sheria Kanda ya Dar es salaam iliyoenda sambamba na Miaka 100 ya Mahakama Kuu iliyoanza Leo kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini humo ambapo ametoa wito kwa wananchi kufika kupata ushauri na msaada wa kisheria bila malipo.

RC Kunenge amesema miongoni mwa elimu itakayotolewa Viwanjani hapo ni pamoja na taratibu za ufuanguaji wa mashauri, Sheria na taratibu zinazotumika katika kuendesha mashauri, ndoa na talaka, utekelezaji wa hukumu, Sheria za Watoto na taratibu za mashauri ya mirathi na Mambo mengine.

Aidha RC Kunenge kwa wananchi watakaofika watapata fursa ya kusikilizwa jopo la Majaji, Wasajili, manaibu Wasajili, Mahakimu pamoja na wadau wa Mahakama wakiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na wadau wengine.

Pamoja na hayo RC Kunenge ameipongeza Mahakama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya Katika kuzipatia majibu changamoto za jamii ambapo amewashauri kuendelea kuboresha huduma ili kupunguza kero za wananchi.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dar es salaam Jaji Lameck Mlacha amesema mahadhimisho hayo yameanza rasmi leo Jumapili na yatafikia tamati January 29 hivyo amewahimiza wakazi wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi.

Mahadhimisho hayo yanatanguliwa na kaulimbiu isemayo Mchango wa Mahakama katika Kujenga Nchi inayozingatia Uhuru, Haki, Udugu, Amani na Ustawi wa wananchi.








 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"