1/15/2021

RAIS WA ZANZIBAR DK MWINYI ATEMBELEA SOKO LA KIMATAIFA LA DAGAA GEITA LEO

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Hussein Ali Mwinyi akitembelea Soko la Kimataifa la Dagaa Kasenda akiwa katika ziara yake Mkoani Geita Wilaya ya Chato na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe. Mashimba Ndaki na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

WANANCHI wa Geita wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia wakati wa ziara yake kutembelea Soko la Kimataifa la Dagaa Kasenda Geita leo 14/1/2021

 

WANANCHI wa Mkoa wa Geita wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akiwahutubia katika viwanja vya Soko la Kmataifa la Dagaa Kasenda Mkoani Geita.

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Machimba Ndaki akizungumza na kutowa maelezo ya Soko la Kimataifa la Dagaa Kasenda wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, kutembelea soko hilo akiwa Mkoani Geita.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Geita katiuka viwanja vya Soko la Kimataifa la Dagaa Kasenda Mkoani Geita Wilaya ya Chato, wakati wa ziara yeke kutembelea soko hilo na kujionea biashara ya Dagaa katika Soko hilo, (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu)

    

0 comments:

Post a Comment