Tuesday, January 19, 2021

RAIS MAGUFULI ASHUHUDIA UTIWAJI SAINI KATI YA SERIKALI NA KAMPUNI YA LZ NICKEL LIMITED KUHUSU UCHIMBAJI MADINI YA NICKEL, KAGERA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 January, 2021 ameshuhudia utiaji saini Mkataba wa Ubia wa Uchimbaji madini aina ya Nickel yanayopatikana wilayani Ngara mkoani Kagera. 

Utiaji saini wa Mkataba huo ulifanywa na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kwa niaba ya Serikali na Bwana  CHRIS SHOWALTER kwa niaba ya Kampuni ya LZ Nickel Limited ya nchini Uingereza. 

Hafla ya utiaji saini ulifanyika katika shule ya Sekondari ya Bukoba na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
 

0 comments:

Post a Comment