1/24/2021

RAFIKI SDO YAUNDA MABARAZA YA WATOTO NGAZI YA KIJIJI HALMASHAURI YA SHINYANGA

 

Mratibu wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutoka Shirika la Rafiki SDO George Nyanda,akizungumza kwenye uundaji wa baraza la watoto katika kijiji cha Shilabela Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


Na Marco Maduhu -Shinyanga. 
Shirika la Rafiki (SDO) ambalo linatekeleza shughuli za utetezi wa haki za wanawake na watoto Mkoani Shinyanga, limeendesha zoezi la uundaji wa mabaraza ya watoto ngazi ya kijiji, katika kijiji cha Shilabela na Pandagichiza, Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Zoezi la uundaji wa mabaraza hayo limefanyika leo Jumamosi Januari 23,2021 kwenye vijiji hivyo, kwa kushirikiana na maofisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, pamoja na Katibu wa MTAKUWWA wa Halmashauri hiyo, kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT). 

Akizungumza wakati wa uundaji wa mabaraza hayo Katibu wa mpango mkakati wa Serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari, amesema mabaraza hayo ni muhimu yatawasaidia watoto kupaza sauti za kupinga ukatili dhidi yao. 

Amesema mabaraza ya watoto ni chombo muhimu, ambapo watakuwa mabalozi kwa wenzao katika kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili, na kutoa taarifa kwa viongozi ili hatua zichukuliwe na kutokomeza vitendo hivyo. 

"Tunaunda mabaraza haya ya watoto ngazi ya kijiji, na baadae tutafika ngazi ya Kata, na wilaya, lengo ni kuwajengea uwezo watoto namna ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa kupaza sauti zao wao wenyewe na kutetea haki zao ," amesema Omari. 

"Matukio ya ukatili ambayo tunapingana nayo sana dhidi ya watoto katika Halmashauri yetu ya wilaya ya Shinyanga, ni vitendo vya mimba na ndoa za utotoni, ambapo wanafunzi wamekuwa wakizima ndoto zao kwa sababu ya kuozeshwa katika umri mdogo na kuacha shule," ameongeza. 

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutoka Shirika hilo la Rafiki SDO George Nyanda, amesema uundaji wa mabaraza hayo ya watoto, ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wao wa kupinga matukio hayo katika Kata ya Pandagichiza na Mwamala Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Amesema mradi huo unaoitwa 'Tuwalee Project', ambao umefadhiliwa na Shirika la Women Fund Tanzania (WFT), ambao utadumu ndani ya miezi minne kuanzia Januari hadi April mwaka huu kwa ajili ya kupunguza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ndani ya jamii. 

Naye mwenyekiti wa baraza la watoto ambaye alichaguliwa na  katika kijiji cha Shilabela Jesca Duma, amepongeza uundaji wa mabaraza hayo, ambayo wamebainisha yatakuwa msaada kwao katika kupigania haki na kutimiza ndoto zao. 

Aidha uchaguzi wa Baraza la watoto katika kijiji cha Shilabela Mwenyekiti amechaguliwa Jesca Duma, Makamu Mwenyekiti Yasinta Emmanuel, Katibu Justina Daudi, na Mwekahazina ni Revocatus Nicolaus. 

Katika kijiji cha Pandagichiza, Mwenyekiti wa Baraza la watoto amechaguliwa Richard Raurent, Makamu Mwenyekiti Felista Gerald, Katibu Adela Charles, na Mwekahazina ni Sarafina Daudi. 

ANGALIA PICHA HAPA CHINI 
Katibu wa mpango mkakati wa Serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari, akizungumza kwenye uundaji wa baraza la watoto katika kijiji cha Shilabela Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha na Marco Maduhu
Mratibu wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutoka Shirika la Rafiki SDO George Nyanda,akizungumza kwenye uundaji wa baraza la watoto katika kijiji cha Shilabela Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mratibu wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutoka Shirika la Rafiki SDO George Nyanda, akiendelea kuzungumza kwenye uundaji wa baraza la watoto katika kijiji cha Shilabela Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Afisa mtendaji Kata ya Pandagichiza Deogratius Mashamba, akizungumza kwenye uundaji wa mabaraza ya watoto ngazi ya kijiji.
Afisa maendeleo ya jamii Kata ya Iselamagazi Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Edmund Ardon, akizungumza na watoto kwenye uundaji wa baraza la watoto ngazi ya kijiji, katika kijiji cha Shilabela.
Afisa maendeleo ya jamii Kata ya Usanda Halima Tendeja, akizungumza kwenye uundaji wa baraza la watoto katika kijiji cha Shilabela, Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Afisa maendeleo ya jamii Kata ya Pandagichiza Stella Prosper, akizungumza kwenye uundaji wa baraza la watoto katika kijiji cha Shilabela kwenye Kata hiyo.
Watoto wa kijiji cha Shilabela wakiwa kwenye uundaji wa baraza la watoto ngazi ya kijiji.
Watoto wa kijiji cha Shilabela wakiwa kwenye uundaji wa baraza la watoto ngazi ya kijiji.
Watoto wa kijiji cha Shilabela wakiwa kwenye uundaji wa baraza la watoto ngazi ya kijiji.
Uongozi wa baraza la watoto ngazi ya kijiji katika kijiji cha Shilabela pamoja na wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kuchaguliwa na watoto wenzao.
Uongozi wa baraza la watoto ngazi ya kijiji katika kijiji cha Pandagichiza pamoja na wajumbe wa baraza hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kuchaguliwa na wenzao.
Mwenyekiti wa baraza la watoto katika kijiji cha Shilabela Jesca Duma, akiahidi kufanya kazi ya kuwakilisha watoto wenzake kupaza sauti ya kupinga matukio ya ukatili dhidi yao.
Mwenyekiti wa baraza la watoto katika kijiji cha Pandagichiza Richard Raulent akizungumza mara baada ya kuchaguliwa na kuahidi kupigania haki za watoto wenzake.
Katibu wa mpango mkakati wa Serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari,akicheza na watoto mara baada ya kumaliza kuunda baraza la watoto katika kijiji cha Shilabela.
Katibu wa mpango mkakati wa Serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari,akicheza na watoto mara baada ya kumaliza kuunda baraza la watoto katika kijiji cha Pandagichiza.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.
    

0 comments:

Post a Comment