Tuesday, January 26, 2021

KAMATI ZA BUNGE ZAENDELEA NA VIKAO


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Humphrey Polepole  akifuatilia uwasilishwaji wa  maelezo kuhusu Muundo na Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  wakati Kamati yake ilipokutana na Wizara hiyo. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bi. Eunice Shirima. 

 


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mheshimiwa Stanslaus Nyongo akisisitiza jambo wakati Kamati yake ilipokutana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupokea maelezo kuhusu Muundo na Majukumu ya Wizara hiyo. Kulia ni katibu wa Kamati hiyo Bi Pamela Palangyo na kushoto ni Mheshimiwa Hamis Taletale.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Seleman Zedi akizungumza katika kikao cha Kamati kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma, katika kikao hicho kamati ilipokea maelezo kutoka Hazina kuhusu uhusiano wa Hazina na kamati ya LAAC

Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakimsikiliza Kamishna wa Bajeti, Ndugu Balandya Elikana wakati akiwasilisha maelezo kuhusu uhusiano uliopo kati ya Hazina na Kamati ya LAAC katika kikao cha Kamati kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.

Msajili wa Hazina Ndugu Athuman Mbuttuka akiwasilisha mada kuhusu Sheria na Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.

 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sheria wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Eustard Ngatale akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati Wizara hiyo ilipowasilisha maelezo kuhusu Muundo na Majukumu yake. Waliokaa kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Festo Dugange  na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerlard Mweli.

Kamishna wa Bajeti, Ndugu Balandya Elikana akiwasilisha maelezo kuhusu uhusiano uliopo kati ya Hazina na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia uwasilishwaji wa  maelezo kuhusu Muundo na Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  wakati Kamati hiyo ilipokutana na Wizara hiyo. 


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Innocent Bashungwa akiwasilisha maelezo kuhusu Muundo na Majukumu ya Wizara yake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizari ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Hassan Abbas.(Picha na Ofisi ya Bunge).

0 comments:

Post a Comment