Thursday, January 21, 2021

Kaimu Katibu Mkuu akutana na Balozi wa Vietnam

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi (kulia) akimsikiliza Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien (kushoto) wakiwa katika mazungumzo yalifanyika katika Ofisi za Wazara jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi (kulia) akimsikiliza Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien (kushoto) wakiwa katika mazungumzo yalifanyika katika Ofisi za Wazara jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akisaalimiana na Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien alipowasili katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma. Wawili hao wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo biashara na uwekezaji baina ya Nchi hizi mbili. 

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi (kulia) na Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Viet Nam na Wizarani mara baada ya mazungumzo. 

Kaimu Katibu Mkuu akutana na Balozi wa Vietnam 

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini Mhe.  Nguyen Nam Tien ofisini kwake jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha mahusiano  ya kidiplomasia yaliyopo kati ya Tanzania na Vietnam na kuona jinsi Tanzania inavyoweza kujifunza na  kunufaika na utaalam na uwekezaji kutoka Vietnam

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu Balozi Mbundi ameelezea kuridhishwa na namna wawekezaji wa kutoka Vietnam wanavyoendesha shughuli zao nchini huku wakifuata sheria za nchi na kulipa kodi kwa wakati na hivyo kusaidia jitihada za Serikali ya Awamu Tano ya kukuza uchumi wa Nchi.

Pia ameelezea matarajio ya Tanzania katika kunufaika zaidi na mahusiano mazuri na Vietnam hususan katika maeneo ya matumizi ya teknolojia katika Kilimo na Uvuvi .

Naye Balozi Tien amesema Vietnam iko tayari kushirikiana na Tanzania katika maeneo hayo ili kuhakikisha maliasili zilizopo Tanzania zinainufaisha nchi na wananchi wake.

Amesema kwa sasa Ubalozi unafanya mazungumzo na wawekezaji wa nchini kwao ili kuona namna watakavyoshirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuanzisha mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Viwanda Tanzania (TCCIA) ili kuwaita wawekezaji wa Vietnam kuja kuwekeza nchini katika viwanda vya kuzalisha korosho nchini hasa ikizingatiwa kuwa Vietnam ni nchi ya pili kwa ununuzi wa Korosho za Tanzania.

  


0 comments:

Post a Comment