Wednesday, January 20, 2021

JOE BIDEN AAPUSHWA RASMI KUWA RAIS WA MAREKANI, TRUMP "AKACHA"

RAIS wa 46 wa Marekani Joe Biden ameanza majukumu ya kuliongoza Taifa Hilo kubwa kabisa Duniani kwa kipindi Cha miaka Minne, baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu wa nchi hiyo mbele ya jengo la Bunge Capitol Hill jijini Washington DC Januari 20, 2021.

Pia Makamu wa Rais Kamala Harris naye ameapishwa kushika wadhifa huo.

Rais aliyemaliza muda wake Donald Trump hakuhudhuria sherehe hizo lakini Makamu wake Mike Pence yeye alihudhuria ikiwa ni pamoja na Marais wote Wastaafu, Bill Clinton, George Bush na Barack Obama.

 

0 comments:

Post a Comment