TANESCO YAWAPANDISHA KIZIMBANI WATU SABA KWA KUINGILIA MIUNDOMBINU YA UMEME

Watu Saba wakazi wa Ukonga, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi kwa kuisababishia hasara Tanesco

Washtakiwa hao ni  Mwalimu Boniphace Singaille(48) Twalibu Kasamu(32), Mwarami Mussa(45), Vumilia Kambi na Haidary Hassan (35).

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mkuu, Materus Marandu akisaidianaia na Kija Luzungana,  mbele ya hakimu  Mkazi Mkuu  Kassian Matembele.

Wakili Marandu alidai, washtakiwa kwa pamoja na wenzao wawili ambao ni wagonjwa wanadaiwa January 2018 eneo la Kichangani Ukonga Madafu,  waliingilia miundombinu inayotumika kutoa huduma muhimu kwa kutoa  mita ya Tanesco kutoka katika kiboksi kinachohifadhia mita na kuifunga moja kwa moja.

Pia, kati ya Januari  18 na Agosti 2020 katika eneo hilo, washitakiwa wote kwa makusudi waliingilia mita ya umeme wa Tanesco na hivyo kuisababishia shirika hilo hasara ya Sh 6,868,910.

Upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika na kwamba wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Matembele alisema kosa hilo linadhamini kwani thamani ya mali wanayodaiwa washtakiwa hao kuisababishia hasara Tanesco ni chini ya Sh 10milioni.

Akitaja masharti ya dhamana, Hakimu  Matembele alisema kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja kutoka Taasisi inayotambulika kisheria, atakayesaini kusaini bondi ya Sh 1milioni.

Mdhamini mwingine anatakiwa kuwa na barua kutoka Serikali ya Mtaa inayowatambulika ikiwa imeambatanishwa na picha ndogo ya rangi( passport).

Washtakiwa wameshindwa kutumiza masharti ya dhamana na kesi hiyo itatajwa tena, Desemba 16, 2020.


Baadhi ya watuhumiwa hao wakisindikizwa na polisi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Desemba 2, 2020.



Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"