11/16/2020

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB) KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi (Mb) wakila Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa kuwa Mawaziri na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho wa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri wa Fedha pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

 


    

0 comments:

Post a Comment