MAKAMU WA RAIS SAMIA AWASILI BOTSWANA KUMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO WA DHARURA WA SADC TROIKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama  Gaborone Nchini Botswana leo Novemba 26,2020 kwa ajili ya kumuwakilsha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika mkutano wa Dharura wa pamoja baina ya SADC, ORGAN TROIKA, Botswana, Malawi na Zimbabwe Nchi  Zinazochangia Vikosi vya Ulinzi  na Amani vya Umoja wa Mataifa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa Nchini DRC unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Novemba 2020 Jijini Gaborone Nchini Botswana.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameondoka Nchi leo Novemba 26,2020 kwenda Gaborone Nchini Botswana kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Dharura wa pamoja baina ya SADC, ORGAN TRYCA, Botswana, Malawi, na Zimbabwe Nchi zinazochangia vikosi vya Ulinzi na Amani vya Umoja wa Mataifa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa Nchini DRC.

Kwenye mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha mkutano huo wa Dharura unatarajiwa kufanyika trh 28 Novemba 2020 Jijini Gaborone Nchini Botswana, umeitishwa kwa Dharura kwa ajili ya kujadili kuhusu hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na kuweza kuona Changamoto mbalimbali zilizo jitokeza katika eneo la Siasa, Ulinzi na Usalama na pia kwa pamoja kuweza kupata utatuzi wa  mambo yatakayobainishwa  kwenye mkutano huo.



 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"