Thursday, September 24, 2020

MILA POTOFU ,UMASIKINI NI KICHOCHEO CHA UKATILI WA KIJINSIA KATIKA JAMII

 

Navaya James ni mtafiti kutoka Shirika la Pingos Forum anasema mafunzo au  mjadala uliodhaminiwa na OXFAM kwa mradi unaoitwa PG2 kati ya Jamii,Serikali,na uliwafikia wanajamii 25 katika vijiji 2 vya Kitue A na Kitue B
Peter Robert  ni Legwanani anasema kuwa ataitumia vyema nafasi yake   kuwaelimisha vijana wenzake juu ya kutambua na kufahamu aina mbalimbali za ukatili pamoja na kujua madhara ya ukatiliMaria James anasema kuwa amejifunza mambo mengi yeye kama mwanamke ambayo yatamsaidia ,ambapo haitakiwi mtu kufanyiwa vitendo viovu kama kubakwa,unyanyasaji katika jinsia zote mbili,kwa watoto wapate haki yao ya msingi haswa ya Elimu
Magreth Thomas ni mkazi wa Kitoi A amelishukuru shirika la Pingos Forum kwa mafunzo hayo kisha ameahidi kuitumia elimu hiyo kuielimisha jamii yake juu ya masuala ya  ukeketeji kwa watoto wa kike na wanawake pamoja na kumwozesha mtoto wa kike kwa ulazima kabla ya umri anasema yeye alikuwa hafahamu kuwa ni  kisheria.
Mshiriki wa mafunzo hayo ndugu Abraham Sakita kutoka kijiji cha Kitwai A yeye anasema kuwa mafunzo aliyoyapata juu ya ukatili wa kijinsia yatamsaidi yeye kuwa mfano bora katika jamii yake kwa kuhakikisha wanawake hawafanyiwi ukatili mfano; mila na desturi mbaya ya kimila  kupigwa,kubakwa.Na.Vero Ignatus,Simanjiro
Mila potofu pamoja  na umaskini unachangia kwa asilimia kubwa ukatili wa kijinsia katika jamiii ,ambapo ukatili ni kitendo anachofanyiwa mtu kwa lengo la kumsababishia madhara au maumivu,huku Ukatili wa kijinsia huwa ni kitendo chochote cha ukatili anachofanyiwa mtu kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia kimwili,kingono au kiuchumi kwasababu ya jinsia yake

Navaya James ni mtafiti kutoka Shirika la Pingos Forum anasema waliendesha mjadala uliodhaminiwa na OXFAM kwa mradi unaoitwa PG2 kati ya Jamii,Serikali,na wao wenyewe ambapo mafunzo haya yalilenga kuangalia fursa zilizopo za kisheria na za kisera kwaajili ya kuhakikisha kwamba haki za wanawake zinaheshimiwa katika jamii zilizopo pembezoni

Amesema kuwa mafunzo hayo yalikusudiwa kufikia watu 25 katika kijiji cha kitwai A na Kiwai B katika wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara, lengo kubwa likiwa ni  kuhakikisha kuwa kunakuwa na usawa katika masuala ya kijinsia ,kwasababu tatizo ni kubwa hivyo  wanawake wa jamii ya wafugaji wa asili pamoja na wawindaji wa asili ,wapo nyuma katika masuala  yote ya kijamii,maendeleo, na hata haki kwa mujibu wa sheria za kitamaduni

Navaya anasema walikusudia mafunzo hayo kuwafikia wanawake ,vijana na wazee wale wanaosimamia sheria za kimila ili nkuhakikisha kwamba habari hizi ambazo ni hitaji la kisheria za nchi zinahitaji waheshimiwe na haki zao zilindwe

''Tunaposema zilindwe tunamaanisha kwamba kwamfano watoto wa kike wanalazimishwa kuolewa chini ya umri unaohitajika kisheria ,ukeketaji,wanawake wengi kwa mume mmoja,kwa ujumla tunavyozungumza masuakla ya jinsia tunazungumza masuala yote yaliyokatazwa kwa mujibu wa sheria''Alisema Navaya

Nyangusi Mathias ni Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri wilaya ya  Shimanjiro  kwa kushirikiana na shirika la Pingos Forum wameweza kutoa mafunzo kwa wawakilishi wa jamiii juu ya ukatili ambapo imeitikia na imeelewa juu ya ukatili,aina za ukatili sambamba na madhara ya ukatili kwao.

Nyangusi anasema  wameweza kutoa mafunzo kwamba ni namna gani wanaweza kutoa taarifa pale watakavyoona ukakitli unatokea kwa jamii,ambapo wametuelewa na wamepokea vyema pia wameahidi elimu hiyo wataitoa katika jamii zinazowazunguka na kwenye mikutano mbalimbali,pia elimu hiyo imetolewa kwa Malegwanani wa vijiji vyote viwili ili wanapokutana katika vikao vyao elimu hii iweze kuwafikia kwa wingi.

Ameshauri kuwa elimu hii iendelee kutolewa kwa jamii,kwa watoto ambao ndiyo msingi wa sasa na wa baadae,ili iweze kuwa endelevu kwani watoto ni rahisi zaidi kuelewa tofauti na wazazi ,wakielewa madhara juu ya ukatili ni rahisi zaidi kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika kwaajili ya kuokoa maisha yao, kwani mara nyingi ukatili wanafanyiwa wao.

Kwa upande wake Josefu Haule Afisa dawati la jinsia na watoto Jeshi la Polisi,kituo cha polisi Orkesmenti wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara:Kwa ujumla wanashirikiana na taasisi nyingi ikiwemo Pingos Forum kwasababu ya kuielimisha jamii haswa ya kifugaji ili kuweza kujikwamua katika ukatili wa kijinsia ambapo wanaelekeza maana ya ukatili kwa upana zaidi na madhara amabayo yanatokea mara baada ya mtu kufanyiwa ukatili

Amesema kuna kitu wamekiona kama wadau kwamba jamii sasa ina mwamko mkubwa wa kuelewa maana na madhara ya ukatili na matokeo ni mazuri ambapo walipokuja kufundisha mwezi septemba jamii imeelewa na elimu hiyo ni vyema ikaendelea kwaajili ya manufaa zaidi .

Peter Robert  ni Leiguanani ambaye kazi yake kubwa ni kuwaelimisha vijana wenzake juu ya kutambua na kufahamu aina mbalimbali za ukatili ,pamoja na kujua madhara ya ukatili ,pamoja na kuelimisha juu ya masuala ya ukeketaji ambapo wao wamekubali kutokomeza ukeketaji katika jamii yao ,pia wamekubaliana kuwaoa wasichana waliosoma na kupata elimu ili waweze kutusaidia sisi pamoja na jamii kwa ujumla

Aidha ameishauri jamii haswa ya wafugaji wa asili na wawindaji wa asili washirikiane na kusaidiana katika kutokomeza ukatili wa kijinsia, katika jamii zao kwani wakifanya hivyo wataweza kusonga mbele katika kujiletea maendeleo wao na Taifa kwa ujumla  

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo ndugu Abraham Sakita, kutoka kijiji cha Kitwai A ,yeye anasema kuwa mafunzo aliyoyapata juu ya ukatili wa kijinsia, yatamsaidi yeye kuwa mfano bora katika jamii yake ,kwa kuhakikisha wanawake hawafanyiwi ukatili mfano; mila na desturi mbaya ya kimila  kupigwa,kubakwa.

Sakita anasema kuwa awali yeye alikuwa hafahamu aina za ukatili ila kupitia mafunzo hayo ameweza kufahamu kuwa mila potofu ni mojawapo,ili  waweze kutokomeza ukatili inabidi kudhibiti mila potofu na kutoa elimu kwa jamiii ili waweze kufahamu madhara ya ukatili pamoja na kuepukana na ubaguzi wa kijinsia,ukatili wa kiafya .

Maria James anasema kuwa amejifunza mambo mengi yeye kama mwanamke ambayo yatamsaidia ,ambapo haitakiwi mtu kufanyiwa vitendo viovu kama kubakwa,unyanyasaji katika jinsia zote mbili,kwa watoto wapate haki yao ya msingi haswa ya Elimu

Magreth Thomas ni mkazi wa Kitoi A amelishukuru shirika la Pingos .kwani amegundua na kuona ukeketeji kwa watoto wa kike na wanawake ni kitendo kibaya,kumwozesha mtoto wa kike kwa ulazima kabla ya umri husika ni kosa  kisheria ,hivyo amesema elimu hiyo itawasidia wao pamoja na jamii inayowazunguka katika kutoa elimu juu ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katikia nyanja zote .

Mwisho0 comments:

Post a Comment